Somo I. Mdo 4:32-35, Somo II. IYn
5:1-6, Injili Yn 20:19-31
Fadhila ya imani ni kushawishika kwa moyo na kweli za KiMungu
bila kutegemea tu ushahidi wa milango
yetu ya fahamu. Ufufuko wa Yesu ni ushindi dhidi ya kifo cha mwili na cha roho.
Ushindi huu unatuingiza katika maisha mapya ya furaha milele, maisha
yasioyoonja taabu ya aina yeyote ile milele yote. Furaha hii ya milele
tutaipata kikamilifu mara ya baada ya kumaliza maisha yetu ya hapa duniani.
Furaha hii inapita furaha zote za ulimwengu huu. Pamoja na kwamba hatujawahi
kuipata furaha hiyo lakini tuamimi kwamba ipo na tutaipata.
Imani ya Tomaso kwa Yesu Mfufuka kadiri ya injili ya leo inategemea tu ushahidi wa
milango ya fahamu. Baada tu ya kumuona Tomaso anamkiri kuwa Bwana wake na Mungu
wake na kuanzia hapo anapata tamanio la kuungannika na Kristu huyu mfufuka na
anaishi kadiri ya tamanio hilo hadi kufa shahidi. Hatuoni kwamba Kristu
amestaajabishwa sana na imani ya Tomaso baada ya ungamo lake. Badala yake
Kristu anawabariki wale wote wanaotamani kuunganika na Kristu kwa kusikia tu
habari zake kutoka kwa watu wengine na sauti ya dhamiri zao bila ya kumuona
wala kugusa madonda yake. Kristu ni kama vile anamwambia Tomaso ikiwa kila mtu
atakayefuata baada ya yeye kwenda mbinguni akahitaji kumuona na kugusa madonda yake ili amwamini hata baada ya kuhubiriwa,
hakutakuwa na waaamini kwani hawatapata nafasi ya kumuona na kumgusa Kristu.
Katika somo la kwanza, Wakristu wa kanisa la kwanza walishawishiwa
juu ya ufufuko wa Kristu kwa mahubiri ya mitume peke yake bila kuhitaji
kumuona wala kumgusa Kristu. Ufufuo wa Kristu ulibadilisha mtazamo wao. Uliwafanya
waamini kuwa maisha ya Mbinguni yana
raha zaidi kuliko raha za dunia hii zinazotokana na mali ingawaje hawajawahi
kuishi mbinguni. Tamanio hili la maisha ya raha ya Mbinugni liliwafanya waone
kuwa si tatizo kwao kufanya kila kitu shirika, kila mtu kutoa mali zake kwa
ajili ya maihitaji ya jumuiya.
Neno la Mungu katika somo la pili linatueleza kuwa imani yetu
kwa kristu, Mungu kweli na mtu kweli, inatufanya tuushinde ulimwnegu. Kristu
aliyekubali kuwa mtu alionja upinzani mkali kutoka ulimwengu huu, nguvu kama
vile mateso, uchungu, umasikini, ubinafsi, mali, zinazotaka ufalme wa Mungu usienee duniani. Yesu
mtu kweli alishinda vita dhidi ya nguvu zote hizi pinzani na daima alikuwa mtii
kwa mapenzi ya Mungu. Yeyote anayemwamini Kristu Mungu kweli na mtu kweli,
aliyeshinda upinzani wote huu katika ubinadamu wake daima atauushinda ulimwengu
katika nguvu zake zote pinzani dhiidi ya mapenzi ya Mungu.
Binadamu kwa hulka yetu tunahitaji ishara ili tuamini jambo
na ndio maana mara nyingi tuko tayari kusoma kwa bidii sana kwa sababu
tunaamini kuwa mafanikio yetu kimaisha yanategemea elimu kubwa. Imani hii
tumeipata kwa sababu tumemuona baba, mama, kaka dada au rafiki aliyefanikiwa
katika masomo. Linapokuja swala la kufanya juhudi kubwa kuachana na vilema
vyetu vya dhambi vinavyotusumbua ili tupate maisha ya raha mbinguni hadithi n
itofauti na sababu kubwa ni kwamba kwa uhakika hatuna mfano tulioona wa mtu
aliyefanya hivyo na sasa anapata raha mbinungi. Tumuombe Mungu atupe paji la
imani tuweze kuamwamini Kristu pasipo kumgusa wala kumuona
No comments:
Post a Comment